Kiasi cha shilingi milioni miatano zilizotolewa na Serikali zimekamilisha ujenzi wa Kituo Cha Afya Kata ya Mundindi,Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi inayo tekelezwa kwenye Wilaya ya Ludewa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sanday Deogratias amesema Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ipo tayari kutekeleza yale yote ambayo Serikali imeyaweka bayana katika kuwatumikia wananchi wake.
Aidha amesema kuwa kwa kukamilika kwa kituo cha Afya hicho ambacho kitatoa adha ambazo wananchi wamekuwa wakizipitia shida kuzipata na sasa zimefikia kikomo.
Sambasamba na hilo nao wananchi ambao wamekuwa ni wahanga wakubwa katika kupokea huduma za matibabu wamempongoza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali yake kwa ujumla kwa kuwaona na kutoa fedha ya kujengea kituo cha Afya ambacho kinaenda kuwasaidia kutokwenda safari ndefu kufuata huduma ya matibabu.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.