Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Bwana Linus Malamba leo Septemba 09, 2022 ameongoza kikao cha wadau wa Kilimo kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere.
Kikao hicho kimehusisha Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ludewa, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Ludewa pamoja na Afisa Tarafa ya Masasi na Mlangali pamoja na Wadau wa Kilimo wanaojulikana kwa jina la My AGRO.
Katika kikao hicho wamejadili mambo mbalimbali ikiwa na namna bora ya kuwafikishia wakulima elimu ya kilimo na kuwafikishia wakulima pembejeo kwa wakati.
Aidha kampuni hizo zimeweka wazi kuwafikia wakulima zaidi ya elfu moja na kuwafundisha na kuwapa pembejeo kwa bei ya Ruzuku ya Serikali haswa katika mazao mbalimbali likiwemo zao la Alizeti na Mbogamboga.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.