Na. Chrispin Kalinga
Mtendaji wa Kata ya Mundindi Bw. Erick Kabuka ametuma salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @samia_suluhu_hassan kwa kuendelea kuipatia kata ya Mundindi fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu, Afya, Maji na Ulipaji wa fidia kwa wananchi wa kata hiyo kwa kupisha mradi wa madini ya chuma Liganga.
Aliyasema hayo Septemba 12, 2023 alipotembelewa na Afisa Habari na Mawasiliano serikalini alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi akitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Tarafa ya Liganga.
Bwana Kabuka amesema, "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameipatia fedha kata ya Mundindi haswa Kijiji cha Njelela ambapo hapo pana mradi wa madarasa mawili ya shule ya Msingi yaliyo gharimu takribani Milioni 67 sambamba na ukarabati wa miundombinu ya Maji, ujenzi wa kituo cha Afya cha Mundindi kilichogharimu zaidi ya Milioni 500 pamoja na ununuaji wa dawa, Kijiji cha Amani kimepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 773 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 9 na mabweni 4 ya shule ya sekondari Mundindi na hivi karibuni Mhe. Rais ameiongezea fedha kata ya Mundindi kwaajili ya ujenzi wa Hosteli moja yenye thamani ya shilingi Milioni 130 na ujenzi wake upo hatua za mwisho".
Aidha, "Kata ya Mundindi tunakila sababu ya kumshukuru Rais wetu Samia kwa fedha nyingi zilizoletwa kwenye kata hii na sisi watumishi tunamuahidi hatuta muangusha kwenye usimamiaji wa miradi hii, na pia nawashukuru Kamati ya Siasa ya chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ludewa kwakuendelea kuwa karibu na miradi hii kwakushirikiana na viongozi wetu akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva na Mkurugenzi wetu Sunday Deogratias". Alisema Mtendaji wa Kata ya Mundindi.
Mtendaji huyo akamaliza kwa kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. @josephzachariuskamonga kwa jitihada zake hadi miradi hiyo inaletewa kwenye kata ya Mundindi akishirikiana na Diwani wa kata hiyo Mhe. Wise Mgina.
#KaziIendee na hakika #inaendelea
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.