Na. Chrispin Kalinga - Ludewa
Kamati ya Siasa Mkoa wa Njombe, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe (MB), Mhe. Deo Sanga, imefanya majumuisho ya ziara ya kamati hiyo, ambayo ilifanyika katika Halmashauri 6 za Mkoa wa Njombe ili kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka wa 2020/2025.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Ndugu Deo Sanga amesema kuwa, "Tumegundua kuwepo kwa changamoto nyingi sana katika sekta ya Elimu hususani ujenzi wa maboma viporo ya Madarasa, ikiwa ni pamoja na sekta ya Afya, ambapo vituo vya Afya na Zahanati hazijakamilika, hivyo Serikali kupitia Halmashauri zote zikamilishe kwa haraka maboma hayo ili wananchi waweze kuhudumiwa kiufasaha".
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amewataka wale wote wanaotakiwa kutimiza wajibu wao Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka amewataka wale wote wanaotakiwa kutimiza wajibu wao ili Serikali iweze kukamilisha miradi yake kwa wakati.
"Hakikisheni mnatimiza wajibu wenu kuanzia ngazi zote ikiwa ni pamoja na kutembelea Miradi ambayo ipo katika maeneo yenu, sio kuishia kujadiliana mihtasari kwenye vikao vyenu vya Halamshauri" Amesema Mhe. Mtaka
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Pindi Chana amewataka watumishi wote wa Serikali kutimiza wajibu wao kikamilifu Ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ni miongoni mwa Halmashauri zilizohudhiria Kikao kazi hicho sambamba na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Kamati za Usalama za Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Wasimamizi wa Taasisi mbalimbali Serikali ngazi ya Wilaya.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.