Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu imeishauri Wizara ya Ujenzi
na Uchukuzi katika ujenzi wa kushirikisha
wadau kutoa vipaumbele kwa miradi ya
barabara za kiuchumi kwa Taifa na ile ya
kimkakati ili kufanikisha malengo makuu
ya Serikali.
Hayo yamesemwa mkoani Njombe
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.
Selemani Kakoso wakati Kamati hiyo
ilipotembelea na kukagua maendeleo
ya ujenzi wa barabara ya Itoni - Ludewa
- Manda (km 211.4), sehemu ya Lusitu
- Mawengi (km 50), inayojerngwa kwa
kiwango cha zege na kuridhishwa na
hatua zilizofikiwa za ujenzi huo.
"Kamati inaangalia miradi ya kimkakati
hivyo Wizara katika mipango yenu
hakikisheni mnazingatia barabara
zitakazokuza uchumi wa Taifa na
kurudisha gharama kwa haraka",
amesema Mwenyekiti huyo.
Mhe. Kakoso ameeleza kuwa ukamilikaji
wa barabara hiyo utaenda sambamba na
ongezeko la mizigo katika Bandari nchini
kwa kuwa katika Mkoa wa Niombe ndipo kwenye uzalishaji mwingi wa mazao ya
misitu, makaa ya mawe ya Mchuchuma
na madini ya chuma cha Liganga na hivyo
kutaongeza zaidi mapato kwa Serikali.
"Mkoa wa Njombe ni mkoa tajiri sana
kwani una rasilimali kubwa ambazo
zinaweza zikatengeneza pato kubwa
la Taifa na GDP ya kwetu kupanda
kwa kiwango kikubwa", amefafanua
Mwenyekiti wa Kamati.
Aidha, Kamati imempongeza Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuendelea
kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu
ya barabara na madaraja kwa wakati na
kufungua uchumi wa mwananchi mmoja
mmoja na kuchochea biashara kati ya
mikoa kwa mikoa na nchi kwa nchi.
"Tumeelezwa kuwa tayari mkandarasi wa
sehemu ya kwanza ya barabara hii kuanzia
Itoni - Lusitu (km 50), ameshakabidhiwa
eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi hii ina
maana kubwa kuwa Serikali ipo kazini
na inaendelea kuifungua barabara hii",
amesema Mhe. Kakoso.
Vilevile, Kamati imeishauri Serikali
kutafuta fedha kwa ajili ya kuunganisha
mkoa wa Njombe na Morogoro kwa
barabara za kiwango cha lami kuanzia
Kibena - Lupembe - Madeke - Mlimba -
Ifakara - Mikumi kwa kuwa ni barabara ya
kiuchumi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.