Leo Machi 21, 2022 Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Ludewa Bw. Gilbert Ngailo ameongoza kikao cha robo tatu ya kamati ya Wilaya ya Kupinga ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake.
Aidha wakati wa kikao hicho PC. Mwanaisha S. Hamisi wa Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi Wilaya ya Ludewa,pamoja na mambo mengine amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Afua za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake kwa kipindi cha kuanzia Mwenzi Januari hadi Machi 2022.Akaongeza kwa kusema kuwa Dawati la Jinsia la Polisi lipo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa hivyo anawaomba wananchi kutoa taarifa za Ukatili kwenye Dawati hilo popote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwenye Vituo vya Polisi.
Kwa upande wake Mjumbe wa kikao hicho Sheikh wa Wilaya ya Ludewa Haruna Rahim amemuomba Kaimu Mwenyekiti wa kikao cha robo tatu ya kamati ya Wilaya ya Kupinga Ukatili dhidi ya Watoto na Mwanamke Ndg.Gilbert Ngailo,kuwa anaomba lianzishwe na Jukwaa la ukatili dhidi ya wanaume wanao fanyiwa ukatili lianzishwe.
Aidha wakati wa majadiliano hayo juu ya ombi la Sheikh Haruna Rahim kuomba kuanzishwe Jukwaa la Ukatili dhidi ya wanaume wanao fanyiwa ukatili lianzishwe, Mjumbe wa Kikao hicho Afisa Mradi wa Mwanamke imara kutoka Shirika la WILDAF Mkoa wa Njombe amejibu ombi la Sheikh Haruna Rahim kuwa Dawati la Jinsia na Watoto ,lipo kwa lengo la kusikiliza na kuchukua hatua stahiki kwa wale walio fanyiwa ukatili,lakini uwepo wa Dawati hilo haimaanishi kwamba wanao takiwa kwenda kupeleka ukatili huo ni watoto na wakinamama tu,Hapana bali Dawati hilo lipo kwaajili ya wote,Ukatili dhidi ya watoto,Wanawake na Wanaume.
Sambamba na hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Ndg. Gilbert Ngailo amewasisitiza wajumbe wote kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waondokane na Ukatili kwa watu wote.Sambamba na hayo akaongeza kwa kusema kuwa tunapo zungumzia ukatili tunazungumzia Ukatili wa Kimwili,Ukatili wa Kiuchumi,Ukatili wa Kihisia na Ukatili wa Kingono.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.