Kaimu Das wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Ludewa akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere jana wakati wa mazishi ya mtu mmoja aliye fahamika kwa jina la Juma Mndoo alipata fursa ya kuwahutubia wanachi wa kata ya Ludewa ujumbe wa Sensa ya Watu na Makazi.
Katika Hotuba yake jana Juni 09, 2022 alisema kuwa, Usiku wa kuamkia tarehe 23 yaani tarehe 22 kila mmoja anapaswa kuwa nyumbani ili aweze kuhesabiwa na akawasihi wananchi wote kubaki nyumbani na familia zao.
Katika hatua nyingine Bw. Linus Malamba akaongeza kwa kuwasihi wazazi na walezi kuwa kila mtu anahaki wa kuhesabiwa hivyo wazazi wote wasiwaficha watoto walemavu kwani na wao wanahaki ya kuhesabiwa.
Aidha akaongeza kwa kusema kuwa Sensa ya mwaka 2022 ni Sensa ya tofouti ukilinganisha na miaka mingine yote, Sensa ya mwaka huu itachukua siku takribani 10 hivyo akawaomba wananchi wote kwa siku hizo 10 kuwa wavumilivu kwa masilahi mapana ya Wilaya ya Ludewa na Taifa kwa Ujumla wake.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.