Mwenge wa Uhuru unaashiria nuru na mwanga.Uliwashwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961.
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 unatarajiwa kuwashwa rasmi Aprili 02, 2022 na Mwenge huo utawashwa katika Mkoa wa Njombe na baada ya hapo kuanza rasmi kukimbizwa kwenye Wilaya za Mkoa wa Njombe na hatimaye kuukabidhi rasmi katika Mkoa wa Ruvuma pale daraja la Ruhuhu lililopo Wilaya ya Ludewa.
Na kwa mwaka huu 2022 mwenge huu utakimbizwa mikoa yote nchini Tanzania na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa unatarajiwa kukimbizwa Aprili 07, 2022.
Mwenge huu unamulika nchini na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale penye dharau.
Sisi wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa tupo tayali kuupokea mwenge wa uhuru kwenye Wilaya yetu na Kuilinda Amani na kudumisha Upendo.
Kila mwaka kuna mbio za mwenge zinazoanzia kwenye mikoa tofauti kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kulinda uhuru, umoja na amani ambavyo vimekuwepo na kudumu.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kutambua umuhimu na wajibu wetu wa kulinda Uhuru Umoja na Amani ndani ya Halmashauri yetu tunasema karibu Mwenge wa Uhuru Wilayani Ludewa,tupo tayali kuiangazia miradi ya kimaendeleo mikubwa iliyo kamilika,inayo endelea na inayo tarajiwa kuanza.
Mwenge wa Uhuru kwa mawaka 2022 unakimbizwa ukiongozwa na kauli mbiu isemayo,SENSA YA WATU NA MAKAZI:SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO,SHIRIKI KUHESABIWA,TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA.
Sambamba na hayo mengi mazuri ya ujio wa mwenge kwenye Wilaya yetu ya Ludewa,Tunaendelea na utoaji elimu kwa kila idara ambapo siku hiyo ya Mwenge unapo wasili kwenye Wilaya yetu ya Ludewa tutatoa taarifa ya namna ambavyo tunaendelea na utoaji elimu na Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI,MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA,MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA,MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA,JINSI WILAYA INAVYO ELIMISHA WANANCHI KUHUSU LISHE,MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA.
Swali liliulizwa kwamba,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021 aliitwa nani? na akaongeza kwa swali hilo hilo la kwanza kuwa mwaka huu 2022 anaitwa nani?
Na katika swali la pili aliuliza kwamba Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022 Utazimwa Mkoa gani? kwa jibu ambalo limewekwa kwenye Website yetu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa?
Mamia ya watanzania wametiririka kujibu swali la kwanza kwa jibu sahihi japo wengi wamekosea namna yakuandika cheo cha mkimbiza Mwenge Mwaka 2021,Niukweli usio pingika kwamba Mwaka 2021 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru alikuwa Ndg.Luten Josephine Mwambashishi kutoka Jeshi la Wanchi Tanzania na katika swali la pili ambalo wengi mmekosa jibu kwa kushindwa kujieleza ulitakiwa ujibu hivi,Kwa mwaka 2022 Ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ilitolewa lakini haikuweka bayana Kiongozi wa Mbio za mwenge hivyo tunatarajia hivi karibuni Serikali itamtangaza kiongozi wa mbio za mwenge.
Na katika swali la pili liliulizwa hivi, Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022 Utazimwa Mkoa gani? kwa jibu ambalo limewekwa kwenye Website yetu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa?
Swali hili wengi wamejaribu kulijibu kwa matokeo chanya na wakakoseshwa na shariti la jibu linalo patikana kwenye Website yetu,Ulipaswa ujibu kuwa,mWENGE WA UHURU KWA KWA MWAKA 2022 UTAADHIMISHA KILELE CHAKE KATIKA MKOA WA KAGERA,WATU WENGI HUJA NA DHANA YA MWENGE WA UHURU HUZIMA NA TAFSIRI YA KUZIMA NADHANI ITAKUWA INAWELEWEKA,NAMI LEO NAKUONGEZA KITU HAPA MWENGE WA UHURU ULIWASHWA TANGU MWAKA 1961 NA MIAKA YOTE TANGU HAPO HUWA TUNAADHIMISHA KILE KILICHO FANYIKA MIAKA YA 60 ILIYO PITA MWENGE ULIWASHWA NA HAUTA ZIMIKA KAMWE KWA ISHARA YA NURU NA MWANGA NA KUZILINDA TUNU ZETU TULIZO NAZO.
Endelea kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii mengi mazuri nakuletea sasa kaa mkao wa kupata swali lingine.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.