Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa SSP. Deogratius Massawe amekabidhi mchango uliochangwa kwa hiyari na askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ludewa kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Lugarawa ambalo hivi karibuni liliteketea kwa moto.
SSP Massawe amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, wao kama Jeshi la Polisi wameona vema kuungana na wananchi katika janga lililojitokeza ili kuhakikisha bweni lililoungua linajengwa kwa wakati na kuanza kutumika kama awali.
Kwa upande wake afisa elimu sekondari wa wilaya ya Ludewa Bw. Michael Hadu amelishukuru jeshi la polisi wilaya ya Ludewa kwa kuungana na wadau mbalimbali waelimu kwa kutoa mchango huo na kuahidi kuzifikisha fedha zote kwa kamati ya maafa kwaajili ya kuendeleza ujenzi unaoendelea.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.