Na. Chrispin Kalinga
Maonesho na Sherehe ya Nanenane mwaka 2023 yamefanyika katika uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya na Katika maonesho hayo waoneshaji walioshiriki ni 574 wakijumuisha Wizara, Taasisi za Umma na binafsi, Asasi za Kiraia, Wabia wa Maendeleo, Makampuni, Taasisi za kifedha, wakulima, wafugaji, wavuvi na waonaji walioshiriki wanakadiriwa kuwa zaidi ya 500,000.
Aidha, Maonesho na Sherehe ya Nanenane hupambwa na ushindanishaji wa wadau wa Sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika na Washindi kupewa zawadi mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imeshika nafasi ya ya kwanza Kitaifa kwa mwaka 2023 katika maonyesho ya nanenane yaliyofanyika tangu tarehe 01 hadi leo 8/8/2023 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahirisha maonyesho hayo.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa upande wa Ufugaji wa Samaki imeshika nafasi pili kitaifa ambapo mfugaji Longinus Mgani kutoka Kata ya Lugarawa Tarafa ya Liganga Wilaya ya Ludewa ameshindanishwa na wagugaji wa Halmashauri zingine na kushika nafasi hiyo.
Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa unawashukuru sana watanzania wote na wasio wa Tanzania kwa kutembelea Banda letu la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na tunawakaribisha tena kwa mwaka ujao ambapo tutakuwa na Mambo mengi mazuri katika banda letu la maonyesho ya nanenane kwa kwa mwaka 2024 yatafanyika katika Jiji la Dodoma.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.