Na Chrispin Kalinga
Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yanalengo la kutangaza vivutio vya Utalii na maeneo ya uwekezaji nyanda za Juu Kusini.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ina maeneo makubwa ya uwekezaji wa viwanda na maeneo ya Utalii, kama uwepo wa Ziwa Nyasa, Mlima Mrefu nyanda za juu Kusini Mlima Livingstone Madunda, Historia ya Makabila ikiwemo kaburi la Chifu Kidulile, udongo wa vyungu vyenye ubora Tanzania, mawe ya Chuma, barabara za kitalii ikiwemo barabara ya kutoka Mbwila hadi Lifuma, pamoja na miti mikubwa ya asili katika mashamba makubwa tofauti likiwemo la Milo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias amesema Kitengo cha Biashara na Uwekezaji pamoja na Eneo la Utalii wamejipanga kuhakikisha kuwa mwekezaji anapofika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa anapata huduma stahili kwa haraka ili aweze kuwekeza kwani kwa kufanya hivyo mapato ya ndani na nchi kwa ujumla yanaongezeka na watanzania wanapata ajira.
Aidha amewakaribisha watanzania kufanya utalii wa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ili kujionea vitu mbalimbali vinavyopatikana Wilayani Ludewa kama Madini ya Chuma, Chokaa na hata Makaa ya Mawe amabayo hivi karibuni Uchimbani unaanza.
Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2023 yamemalizika leo katika viwanja vya Kihesa Kilolo yaliyozinduliwa tarehe 23/09/2023 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Angellah Kairuki(MB) ambapo Mikoa 10 imeratibu Maonesho hayo ya Utalii Karibu Kusini na waoneshaji zaidi ya 130 wameshiriki.
Na leo tarehe 28 Septemba 2023 yamehitimishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.