Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imepokea Fedha za Ujenzi wa Ofisi Mpya za Halmashauri hiyo kongwe Nchini kutoka Serikali Kuu. Mradi huo ni moja kati ya miradi mingi ambayo inatekelezwa Nchi nzima katika Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Jemadari Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Mradi huo unaotekelezwa na Wataalamu kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Katika kuhakikisha mradi unaanza na kukamilika kwa wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa amefanya makabidhiano ya eneo la Ujenzi mapema leo Ijumaa tarehe 19 Januari, 2021 ambapo kikao cha makabidhiano kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Bi. Gladness Mwano akiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo wote, na kwa upande wa mjenzi wa mradi uliwakilishwa na Wahandisi Stephano Maduka na Moses George Moyo kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) cha Mbeya. Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Gladness Mwano amewataka wataalamu kutoka MUST kuzingatia muda wa utekelezaji wa mradi kwani kama wamiliki wa mradi, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa inawaamini kwa uwezo na utaalamu wao kwani ni Taasisi ya Umma hivyo wanauzoefu wa matumizi ya Fedha za umma na uzingatiaji wa muda wa utekelezaji wa miradi ya Serikali. Aidha, nao wataalamu hao kutoka MUST wamewahakikishia wajumbe wa kikao hicho kwamba wao wanao uwezo mkubwa wa kutimiza wajibu wao na hivyo kuomba ushirikiano zaidi ili kutimiza azma yao ya kujenga jengo hilo la ofisi kwa wakati uliokubalika.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.