Na. Chrispin Kalinga
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wa Wilaya ya Ludewa, Ndg. Gervas Ndaki wakati amewaeleza wananchi wa kata ya Mundindi utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 katika mkutano wa wazi wa mkuu wa Wilaya ya Ludewa uliokuwa umewakusanya wananchi wa kata hiyo kwaajili ya uzinduzi wa Zahanati ya Chimbo na upokeaji vifaa tiba na dawa zilizonunuliwa za kituo cha Afya Mundindi amesema kuwa, wananchi wasikubali kudanganywa na watu juu ya utekelezwaji wa miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa katani hapo na kudai kuwa Kata ya Mundindi imepokea fedha nyingi za utekezaji w miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi ya Elimu, Afya na Maji.
Ndaki amesema kuwa, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mingi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Kila mahali na sekta serikali inatekeleza miradi ya kimaendeleo.
Aidha akasema, "Wakati wa kampeni thlipita hapa na kuomba kura kwenu wananchi, na tukaahidi kujemga kituo cha Afya Mundindi na leo kituo hiki hapa kinaonekana kikiwa kimekamilika na tayari serikali imeajiri watumishi kituo kinatoa huduma, na Bado leo Mkuu wa Wilaya amekagua vizaa,dawa zilizonunuliwa na ameagiza hapa huduma ziendelee, niwaombe Ndugu zangu sisi ndio wa kuyasema haya kwa vitendo, mtu akija hapa akisema serikali imefanya nini mleteni hapa kwenye kituo cha Afya, mpelekeni Mundindi kwenye Madara 9 mpelekeni shule ya watu wenye nahitaji maalumu akashuhudie utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi iliyotekelezwa kwa kishondo" Alisema Ndaki.
Yote hayo yameongelewa Jana Septemba 12, 2023 wakati wa mkutano wa wazi uliofanyika kata ya Mundindi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.