Habari kubwa katika Jarida letu la leo ni jengo la Ofisi kubwa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa linalo jengwa katika Halmashauri hiyo huku ujenzi wake ukiendelea kwa kasi ukilinganisha na kipindi kilicho pita kwa sababu ya mvua kubwa zilizo kuwa zikiendelea kunyesha.
Kukamilika kwa jengo hilo litatatua kero ya ukosefu wa Ofisi za idara mbalimbali zilizotawanyika.
Lakini pia Ukamilikaji wa jengo hilo litakuwa ni jengo zuri ambalo litawavutia watu wengi kuja kulitembelea kutokana na uzuri wa jengo lenyewe na wengi watatamani kupiga picha katika eneo hilo.
Aidha katika jarida letu la leo habari kubwa iliyo gusa mioyo ya watu wengi ni kutoka pale Kata ya Luana ambapo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg.Sunday Deogratias aliwaahidi wananchi wa Kata ya Luana alipo kuwa akiwahutubia katika mkutano wa wawazi na kusema kuwa, Kata ya Luana ni miongoni mwa kata zinazo fanya vizuri haswa katika ukelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasà, Ujenzi wa vituo vya afya nk.
Hivyo kwa uunga mkono jitihada za wananchi wa Kata hii sasa nikiwa Kama Mkurugenzi nitatoa Bati 176 ambazo Mhe. Diwani Wilbard Mwinuka ameniomba.
Hivyo nawaombeni wananchi tuendelee kuiunga mkono serikali yetu kwa kuendelea kufanya kazi ili tutekeleze miradi yote inayo endelea kwenye kata hii "alisema Sunday Deogratias Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Ludewa" kauli hiyo aliitoa Mei 29, 2022.
Licha ya Miradi mingi inayo tekelezwa kwenye Wilaya ya ludewa, Diwani wa Kata ya Ludende Mhe. Vasco Mgimba akishirikiana na wananchi wa Kata hiyo wamefanikiwa kuinua jengo la Mama na mtoto la kituo cha Afya cha Ludende ambao Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilitia mkono wake kuunga mkono juhudi za wananchi, lakini pia Diwani wa Kata hiyo bado amenyenyekea chini ya serikali kuomba kuungwa mkono ili kukamilisha jengo hilo ambapo awali serikali ilitupia mkono wake katika hengo hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ludewa bado amewapa Imani kubwa wananchi wa Kata hiyo kwa kusema kuwa,
Serikali inatambua mchango mkubwa wa wananchi wa Kata hiyo ndio maana Walipo omba Halmashauri isaidie kwa awamu ya kwanza ilitekeleza na kwasasa Mhe. Diwani kaomba tena na sisi Kama Halmashauri tutaaungana na wananchi kukamilisha jengo hilo kwa Bajeti ya Mwaka 2022/2023.
Katika hatua nyingine katika jarida letu la leo Juni 02, 2022 Sehemu ya juu inaelezea Ujenzi wa chuo cha Ufundi VETA kinacho jengwa Kata ya Lugarawa pale shaulimoyo, ujenzi wake unaendelea na kwasasa upo kwa asilimia 20% ambapo ukamilikaji wake ni mwishoni mwa mwaka huu, na kusuasua kwa mradi huo ni kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha kwa kipindi cha mwezi January hadi Aprili.
Pia neema nyingine yamwagika tangu kuumbwa kwa ulimwengi barabara ya kutoka Mbwila hadi Lifuma inaendelea na uchimbwaji ambapo kukamilika kwa barabara hiyo itakuwa imeokoa gharama kubwa za usafiri ukilinganisha na wakati huu wananchi hulazimika kusafiri kwa kutumia Ziwanyasa (Mitumbwi na Boti)
Jitihada za Mhe. mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga zinaendelea kuzaa matunda, na ikumbukwe kwamba Jana Mei moja aliweza kuhoji Bungeni mambo mbalimbali ikiwemo uendelezwaji wa nguvu
za wananchi wake.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.