Katika Jarida letu la leo ukiondoa habari kuu yagazeti letu Leo nimekusogezea taarifa mbalimbali kutoka ndani ya Wilaya yetu.
Na moja ya habari hizo ni pamoja na Jeshi la Polisi Wilaya Ludewa linaendelea kupaza sauti kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kuwapa elimu ya Ukatili wa kijinsia na kuwasihi watanzania wote wa Wilaya ya Ludewa kuachana na vitendo vya kikatili ambavyo hivyo hupelekea vifo.
Aidha Inspector Violeth GIdeon amepaza sauti kwa kuzifikia Tarafa zaidi 3 za Wilaya ya Ludewa kwa kuendelea kuelimisha na Kuhamasisha kutokomeza Ukatili wa kijinsia huku akibainisha kwa kuwapa uhuru wananchi wote kutoa taarifa za ukatiki wanapo ziona katika kituo chochote cha Polisi.
Wananchi hupata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa ufumbuzi na huku Inspector huyo akiwasihi wanawake kuacha Ukatili kwa watoto na kwawaume zao na akawasihi wanaume kutoa taarifa katika Dawati la jinsia pindi wanapo fanyiwa ukatili na wanawake zao.
*"Nitumie nafasi hii hadhimu kuwasihi wanaume,msione haya kuja kutoa taarifa ya Ukatili pindi mkeo anapo kukatili nenda kituo cha Polisi Dawati la jinsia litakusikiliza na kutafuta suluhisho la tatizo hilo nakuwafanya muishi kwa Amani na Upendo."* alisema inspector
Pamoja na hayo mengi bado katika Jarida letu limetoa taarifa ya elimu ya lishe,ambapo hapo tunakumbushwa kuwa mlo bora kwa watoto wetu itasaidia kuondokana na Udumavu ambao kwasasa kwa Halmashauri yetu ya Ludewa tunataka kuutokomeza kabisa Udumavu.
Katika hatua nyingine hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias alitangaza ajira 8 na mwisho wa kutuma barua za maombi ya kazi ni tarehe 08/06/2022 hivyo watanzania wote mnakumbushwa kutumia fursa hii kwa siku zilizo salia kuomba kazi.
Hali kadhalika wananchi wa Kata ya Milo Wilayani Ludewa wametoa hisia zao kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuziinua kaya masikini kwa Kuziwezesha fedha ambayo imewafanya maisha yao yabadilike.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mapogoro katani Milo wamesema TASAF imewawezesha na kufikisha kujiinua kiuchumi hukubwengi wao fedha hiyo wakiielekeza kwenye Mashamba na wengine wamenunua mifugo na kuifuga na kukarabati nyumba zao.
Lakini pia Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias ametuma salamu za pongezi kwa Kata ya Madilu kwa kuonesha ukomovu na shauku kubwa ya maendeleo ya Wilaya haswa katika eneo la elimu kwa kufanikiwa kujenga nyumba ya mwalimu wa shule ya msingi Madilu ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika mwaka huu.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.