Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday N. Deogratias amekabidhi ofisi rasmi kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Gilbert Ngailo.
Zoezi hilo lilifanyika Jana Februari 04, 2023 na kushuhuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Ludewa akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Wise Mgina, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Daniel Ngalupela. Pia Wakuu wa Divisheni na Vitengo wote wa halmashauri ya wilaya pamoja na watumishi wa kada zote za Halmashauri.
Wakati akitoa salamu za zake za kuwaaga watumishi Ndg. Sunday Deogratias alisema; "Nianze kwa kumshukuru Mungu wakati wote alinisimamia katika nafasi ya Utumishi wangu kwa nafasi ya Ukurugenzi hapa Ludewa kwa miaka yote 4. Pili naomba nimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini wakati wote nilipokuwa hapa Ludewa na hadi leo naondoka Ludewa ikiwa ipo Salama, na mwisho niwasihi watumishi wenzangu tuendeleeni kufanya kazi na kuwapa ushirikiano viongozi wote wateule wa Mhe. Rais".
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Wise Mgina alimshukuru sana Ndg. Sunday Deogratias kwa utumishi wake kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na alimsihi aendelee kufanya kazi Kama alivyokuwa anafanya kazi Ludewa kwa Uwekezaji na majukumu mengine atakayopangiwa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.