Wakati ukijiuliza wapi zinapatika fursa za kilimo hapa nchini Tanzania leo nakunong'oneza kwa ukaribu kuwa Halmashari ya Wilaya ya Ludewa inamaeneo ya mengi ya wazi kwaajili ya kilimo.
Na ikumbukwe kwamba Udongo wa Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa hauchagui zao lipi la falaa kwa kilimo jibu ni kwamba mazao yote yanastahili ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Hivi karibuni Meneja wa Kanda za juu Kusini Bw.Ferouz Mkongo alitembea baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na kushuhudia haya ninayo kueleza.
Bw.Ferouz Mkongo alisema lengo kubwa la kutembelea maeneo hayo ni pamoja na kuwasaidia wakulima wa zao la Kahawa,Korosho,Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa na samaki kupatiwa mikopo ya asilimia 9 kwa mwaka kwenye minyololo ya thamani ya mazao tajwa hapo juu.
Katika kufanikisha hayo Bw. Ferouz aliambatana na Kaimu Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Ludewa Clementina Kabaka na moja ya wakulima walio fikiwa ni pamoja na Mkulima wa Kijiji cha Lufumbu ambaye pia ni mkulima bora wa zao la Kahawa
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.