Wataalamu na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wameshiriki katika mafunzo ya namna ya kuandaa nyaraka za Usimamizi wa Viashiria Hatarishi vya udanganyifu katika Ukumbi wa Idara ya Kilimo. Mafunzo haya ambayo yameratibiwa na Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, yamesimamiwa na Afisa Usimamizi wa Fedha (FMO) kutoka Sekretariati ya Mkoa wa Njombe Bwana Eliuteri Mworia, Bi Christina Minja, wakaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe na Ludewa.
Mafunzo yamehusisha wataalamu kutoka Idara zote za Halmashauri ili kuwezesha kila Idara kuwa na Mratibu wa Kutengeneza mpango, ambao utawasilisha kwa mratibu wa ngazi ya Wilaya. Akizungumza katika mafunzo hayo, Mratibu wa Mpango Wilaya Bwana Onesmo Ngimba amewashukuru wawezeshaji kwani mafunzo yamekidhi hitaji la Halmashauri ambapo na wao kama Halmashauri ya Ludewa walipanga kuwezesha watumishi wa Idara zote ili iwe rahisi kuandaa nyara nzima ya mpango wa Halmashauri.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.