Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo, tarehe 17 Februari 2025 amefanya ziara ya kutembelea miradi ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe katika eneo la Ketewaka na Mchuchuma, Wilayani Ludewa mkoani Njombe. Ziara hiyo ni muhimu katika kuonyesha juhudi za Serikali za kukuza sekta ya viwanda na uchumi kupitia rasilimali za madini, hususani makaa ya mawe ambayo ni chanzo kikubwa cha nishati na maendeleo ya viwanda nchini Tanzania.
Mbali na kutembelea miradi hiyo ya uchimbaji, Mh. Jafo pia amekagua mradi wa uchongaji wa barabara katika mlima Kimelembe. Barabara hii itarahisisha usafirishaji wa madini hayo na kuboresha miundombinu katika wilaya hiyo, jambo litakalosaidia katika kukuza biashara na maendeleo ya uchumi katika mkoa wa Njombe.
Katika ziara yake, Mhe. Jafo pia alifanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Nkomang’ombe, Wilayani Ludewa. Mkutano huo ulijumuisha mazungumzo kuhusu fursa zinazopatikana kutokana na mradi wa madini ya makaa ya mawe na jinsi ya kuhakikisha manufaa ya mradi huu yanawafaidisha wananchi wa maeneo husika. Waziri alisikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kutoa maelekezo ya kutatua baadhi ya matatizo yanayozikabili jamii.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.