Afisa Lishe wa Wilaya ya Ludewa Bw. Mwitambe Samsoni Jana Machi 20, 2023 amekamilisha zoezi la utoaji elimu kwa Tarafa 3 za Wilaya ya Ludewa ikiwa ni pamoja na Tarafa za Mawengi,Masasi na Tarafa ya Liganga.
Katika utoaji wa elimu ya Lishe aliambatana na na watumishi wa idara ya Afya pamoja na Viongozi wa serikali za mitaa akiwemo Watendaji wa Kata, Watendaji wa viijiji husika.
Elimu iliyotolewa kwa wazazi na Walezi wa watoto ni pamoja na namna bora ya mchanganyiko wa vyakula kwa ajili ya kupambana vikali na udumavu.
Aidha wakati akitoa elimu kwa Wazazi na Walezi aliwaelekeza kuwa, licha kuwa bize na shughuli za kila siku kuna haja ya kuzingatia Lishe kwa watoto wao ili waendelee kutokomeza udumavu Kwa watoto maana mtoto mmoja akipata udumavu kwenye familia ni hasara kubwa Kwa familia na taifa Kwa ujumla.
Bw. Samson aliyasema hayo alipokuwa katika uwanja wa zahanati ya Kijiji cha Mbwila na kuongeza kwa kusema kuwa, Wilaya ya Ludewa imejipanga vyema kuendelea kutoa elimu ya Lishe kila Kijiji cha Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na ifikiapo Juni 30, 2023 wanatarajia kuvimaliza Vijiji vyote.
Pamoja na hayo aliwaomba kubadili mwenendo mzima wa uendeshaji wa siku ya Afya na Lishe ya vijiji kwa kuwekana wazi kuhusu suala la udumavu Kwa watoto wao na kuweka mikakati thabiti ya kutokomeza kwani vyakula wanavyo na elimu imekuwa ikitolewa Kila siku.
"Kwenye udumavu hakuna kuficha,tunatakiwa kutoa taarifa ya mtu ambaye hajari mtoto wake katika suala la kumpatia chakula sahihi maana tunawajua na tunaishi nao majumbani mwetu.
Mwisho afisa lishe aliwakumbusha akina mama wote kuzingatia vyakula makundi matano ili kuondoa udumavu maana huanzia tumboni mwa mama akiwa mjamzito kama hapati vyakula vyenu makundi matano na kuendekea na ushauwishi kwa akina baba kuhudhuria siku ya afya na lishe ya Kijiji maana ni muhimu sana katika suala zima la kuondoa udumavu.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.