Na. Chrispin Kalinga
Diwani wa Kata ya Mlangali wilayani Mkoani Njombe Mheshimiwa Hamis Kayombo apongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya kata ya Mlangali.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara ya Afisa Habari na Mawasiliano serikalini Bw. Chrispin Kalinga ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Tarafa ya Mlangali.
Aidha, Mhe. Kayombo amesema kuwa, serikali imetoa fedha za kutekeleza ujenzi wa kituo cha Afya Mlangali ambacho kwa Sasa tayari kinatoa huduma Bora kwa wananchi wa kata hiyo na wananchi wa maeneo ya jirani na akaongeza kwa kusema kuwa licha ya ujenzi wa madarasa ya shule za Msingi na sekondari kukamilika katika kata hiyo sasa serikali imefanikiwa kuongeza kipande cha lami kutoka barabara ya ndani ya kata hiyo.
Mhe. Hamis Kayombo amepiga magoti kwa istara ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuitenda haki kata yake kwa utekelezwaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye kata hiyo sambamba na ukarabati wa miundombinu ya umeme iliyokuwa ikisumbua miaka Mingi kwa mgao na kwa sasa umeme unakuwepo masaa 24.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.