Na. Chrispin Kalinga
Diwani wa kata ya Makonde Mheshimiwa Chrispin Gowele amekuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kudumisha Utamaduni uliokusanya ngoma mbalimbali za asili kutoka Mwambao ikiwemo ngoma ya KIHODA, lengo la michezo hiyo ilikuwa ni kudumisha Utamaduni na kuwahamasisha wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Kimaendeleo zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kata ya Makonde.
Aidha, Mhe. Gowele ametuma salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kuteketeza Miradi katika kata ya Makonde ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wa nyumba za walimu na uboreshaji wa zahanati iliyopo Katani hapo.
Kwa upande wa wananchi wa kata ya Makonde wamempongeza Diwani huyo kwa kuona umuhimu wa kuwakutanisha wananchi wa kata hiyo kushiriki michezo na baadaye kusomewa taarifa ya Maendeleo ya Kata hiyo ambayo iliwasilishwa na Diwani wao.
"Mhe. Diwani tunapenda kukushukuru sana kwakuona umuhimu wa kutukutanisha hapa leo, maana michezo hii hutukutanisha na Marafiki zetu lakini pia tunapokusanyika katika Maeneo Kama haya tunabadilishana mawazo baina ya Kijiji kimoja na Kijiji kingine, na kubwa zaidi tunakushukuru Mbunge wetu Kamonga kwa kipindi alichopo madarakani Makonde umeme umewaka Tunaomba tufikishie salamu hizi na tunamuomba aboreshe Mawasiliano ya simu lakini pia Barabara ya kutoka Mawengi ikamilike ili Makonde yetu iwe rahisi kusafirisha mazao yetu ya Samaki" alisema Mwananchi
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.