Na. Mwandishi wetu.
Diwani wa Kata ya Ludewa Mhe. Monica A. Mchilo leo Septemba 11,2023 ameongoza mkutano wake wa wazi uliokusanya wananchi ya kata hiyo na kuwahabarisha habari njema ya mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita inayoongwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakati akisoma taarifa ya mapato na matumizi pamoja na utekelezwaji wa miradi iliyotekelezwa kwenye Kata ya Ludewa amesema, " Tunakila sababu ya kumshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali kwenye kata yetu, na sisi kata ya Ludewa tulipata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali kiasi cha shilingi Milioni 645,607,600 na fedha hizo zilielekezwa kuboresha na kujenga miundombinu ya shule za shule Msingi na sekondari" Alisema Monica.
Aidha, aliongeza kwa kusema, "nisipo washukuru ninyi wananchi wa kata hii ya Ludewa nitakuwa nakosea Sana, serikali ilitoa fedha na ninyi wananchi mukamuunga mkono Rais wetu kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo lakini pia wakati Msingi mlichangiana kwa lengo la kukamilisha miradi hii asanteni sana wananchi wenzangu na Mimi Kama diwani nipo pamoja nanyi". Alisema Diwani Monica Mchilo
Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa divisheni wa kata hiyo wakiongozwa na Afisa Mtendaji wa kata ya Ludewa Bw. Alanus Mbunda.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.