Diwani wa Kata ya Luana Wilayani Ludewa Mheshimiwa Wilbard Mwinuka leo Julai 05, 2022 amefanya ziara ya kukagua uchimbwaji wa barabara inayotoka Mbwila hadi Lifuma.
Wakati akiendelea na ziara yake ya ukaguzi wa barabara hiyo diwani huyo amesema kuwa, barabara hiyo ya kutoka Mbwila hadi Lifuma inaendelea vizuri na takribani kilomita 5 kutoka inapochepuka hadi eneo la Malovi imechimbwa.
Aidha Diwani huyo akaongeza kwa kusema kuwa "Nawapongeza sana wananchi wa kijiji cha Mbwila pamoja na viongozi wao kwa ushirikiano kwa kuendelea kutembelea mradi huo mkubwa na muhimu mara kwa mara".
Sambamba na hayo Mhe. Wilbard Mwinuka ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe.Joseph Kamonga kwa kuunga mkono juhudi za wanchi kwa uchimbaji wa barabara hiyo na akaongeza kuwashukuru TARURA Wilaya ya Ludewa kwa kujitoa na kujibiidisha katika barabara hiyo huku akisema kuwa wananchi wa maeneo hayo wawe wavumilivu kwa kipindi hiki kifupi barabara inapo chimbwa.
Katika hatua nyingine Diwani huyo amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza mzunguko wa fedha kwenye kata yake ukilinganisha na wakati huu kwani barabara hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo usafari, vyakula nk.
https://www.instagram.com/p/CfoWa94NduW/?igshid=YmMyMTA2M2Y=
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.