Na. Mwandishi wetu - Ludewa
Diwani wa Kata ya Ibumi Mheshimiwa Edward Haule amesema kujengwa na kukamilika kwa Daraja la mto Ruhuhu (IGUGU) litapelekea kuongezeka kwa mzunguko mkubwa wa biashara kati ya mkoa wa Njombe na mkoa wa Ruvuma.
Ameyasema hayo Jana wakati wa ziara yake ya kukagua Barabara ambayo atatakiwa kupita mbunge na viongozi wengine wa serikali wakati wa kwenda kumkabidhi mkandarasi tenda ya ujenzi wa Daraja hilo.
Aidha, Mhe. Haule amekagua Barabara hiyo kuanzia makao makuu ya kata ya Ibumi mpaka eneo ambalo Daraja litajengwa na kuona baadhi ya changamoto ambazo zipo na kuelekeza viongozi wa vijiji kufanya marekebisho yaliyopo kabla ya September 21.2023.
Lakini pia ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2.9 kwaajili ya ujenzi wa Daraja hilo huku akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga kwa kuendelea kuipigania kata ya Ibumi.
Pamoja na hayo ameelekeza pongezi Kwa Meneja wa Tarura wa Wilaya ya Ludewa kwa namna wanavyoendelea kuonyesha ushirikiano wa dhati katika mapambano ya ujenzi wa Daraja hilo.
Pia Diwani huyo amesema taratibu za kikandarasi ziko hatua za mwisho kilichobaki ni mkandarasi kukabidhiwa Kazi na kuanza.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.