Leo tarehe 17 Aprili 2023 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa akiwakilishwa na Ndg. Castor Kibasa ameongoza kikao cha kudhibiti Ukatili dhidi ya Mwanamke na Watoto.
Kikao hicho kimehudhuliwa na wajumbe mbalimbali wa kikao hicho ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi Wilaya ya Ludewa.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili namna bora ya upatikanaji wa taarifa kwa wanafunzi wa shule wa za Msingi na Sekondari.
Akizungumza katka kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Castor Kibasa amesema kuwa, Unyanyasaji kwa wanafunzi mashuleni upo na unyanyasaji huo umekosa mahali sahihi kwa kutoa taarifa lakini pia Usalama wa mwanafunzi mtoa Taarifa, kupitia kikao hiki tuwaombe wanafunzi wote watoe taarifa za Ukatili mashuleni kupitia sanduku za maoni zilizopo katika Shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Sambamba na hayo shule zote zikiunda tume za wanafunzi za ufuatiliaji wa taarifa za Ukatili mashuleni zitakazo kuwa zinaripoti.
Aidha katika kikao hicho kumewasilishwa taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa Ukatili wa kijinsia wakiwemo
1. Kitengo cha Ustawi wa Jamii
2. Polisi Dawati
3. Miso
4. Paralegal
5. Lupao
6. Mahakama
7. Afisa Elimu Msingi
8. Afisa Elimu Sekondari
9. Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.