Na Mwandishi Wetu @hludewa
Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Chrispin Kalinga ameshiriki kikamilifu Kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini, 2023 kilichoanza tarehe 27 Marchi 2023 na kufungwa rasmi leo Machi 30, 2023 na Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Tabia katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Katika Kikao hicho zaidi ya Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini 500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameshiriki kikamilifu.
Ikumbukwe kwamba Kikao hicho kilifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Machi 27, 2023.
Pamoja na mambo mengine Maafisa Habari hao wamekumbushwa kuendelea kutekeleza vyema majukumu yao ya kiutendaji wa kila siku katika maeneo yao kwa kuwahabarisha wananchi Mambo mbalimbali ya kiserikali.
Aidha kesho tarehe 31 Machi 2023 Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini watatembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa ya Umeme (SGR).
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.