Meneja Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za Umma Mkoani Njombe Ndugu Anthony Kilale amefanya ziara ya ufuatiliaji wa uboreshaji wa muonekano wa Tovuti. Katika ziara hiyo ameambatana na Mtaalamu wa TEHAMA kufuatilia kuona namna maboresho yalivyofanyika na kuboresha zaidi. Ziara hiyo ilimefanyika tarehe 26 mwezi wa nne mwaka huu 2016, ilihudhuliwa na maafisa Tehama wote watatu waliopo katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ludewa. Waweza pia kuitazama tovuti hiyo kupitia anwani ifuatayo;
Akizungumza katika majadiliano hayo, Ndugu Kilale amewaasa Mafisa TEHAMA kuhakikisha tovuti inajaa habari zinazowahusu wananchi moja kwa moja ili waweze kuona umuhimu wa uwepo wa Tovuti hii, kwani Serikali kwa kushirikiana na Wafadhiri wa Mradi mabao ni Watu wa Marekani (US-AID) imetumia gharama kubwa na rasilimali kuhakikisha wananchi wanafikiwa na taarifa kwa haraka zaidi mahali walipo. Pia amewaasa kulipeleka suala la Tovuti kwa Waheshimiwa Madiwani ili waweze kuwajulisha wananchi uwepo wa chombo ambacho wanaweza kukitumia kuwasilisha malalamiko yao pia kwa ngazi za Juu katika Halmashauri yao na Wilaya kwa Ujumla.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.