Thursday 21st, November 2024
@Wilaya ya Ludewa-Songambele
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mheshimiwa Andrea Axwesso Tsere kesho Jumamosi August 31, 2019 anatarajia kuongoza mamia ya wakazi wa
Wilaya ya Ludewa katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule maalumu ya vipaji katika Wilaya hiyo. Uzinduzi huo katika hatua za awali
unatarajia kushuhudia shughuli za kusafisha eneo la ujenzi wa shule katika eneo la Songambele kata ya Ludewa.
Akitangaza mchakato wa zoezi litakavyoendeshwa, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa Bi. Zaina M. Mlawa
amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za kujiletea maendeleo sisi wenyewe kwa kufanikisha
ujenzi wa Shule hiyo kwani itakuwa ni kwa faida ya Wana Ludewa wenyewe. Amewaasa wananchi wa Kata ya Ludewa kufika
katika eneo la ujenzi wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi kama vile makwanja, mapanga na reki kwa ajili ya usafi huo kuanzia
majira ya saa mbili kamili asubuhi. Aidha amesisitiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwani ni sehemu ya siku maalumu
ya usafi wa kila mwezi kama ilivyo utaratibu wa usafi kila mwisho wa mwezi. Katika mradi huo wa ujenzi wa Shule maalum
kulikuwa na zoezi la harambee ya kuchangia ujenzi ambapo mpaka sasa kiasi cha Tshs. milioni arobaini na moja (Tsh.41m) zimepatikana.
Ambapo akitoa tathmini, Mkuu wa Wilaya amesema fedha hii inatosha kwa wastani kujenga vyumba viwili vya madarasa, hivyo wadau
zaidi wanaombwa kuendelea kuchangia ili kufanikisha azma hii. Zoezi hili ambalo mchakato wake ulianza mapema mwezi Februari, 2019
litakuwa endelevu na wadau wote walioshiriki na kutoa ahadi anawapongeza kwa ahadi zao ambazo zitasaidia kufanikisha lengo hili.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Sunday Deogratius amewataka watumishi wote waliopo katika
kata ya Ludewa wakiongozwa na wakuu wao wa Idara na Vitengo kuhakikisha wanashiriki zoezi hilo ili kuwatia moyo
wananchi wao wanaowatumikia. Amesema ni ishara nzuri ya umoja, ushirikiano na mshikamano ambao watumishi
wa umma na wananchi wa Ludewa wamekuwa wakishikamana muda wote kwenye masuala ya msingi kama haya.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.