Saturday 18th, October 2025
@Ludewa
1. MAJUKUMU NA KAZI ZA MEYA/MWENYEKITI WA HALMASHAURI, MADIWANI, WENYEVITI WA VIJIJI, MITAA NA VITONGOJI.
1.1 Kwa mujibu wa ibara ya 145 na 146 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za Mitaa ni vyombo vya haki na vyenye mamlaka ya kushiriki na kushirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma katika sehemu zao. Serikali za Mitaa huanzishwa kwa madhumuni ya kuwahudumia wananchi na kuwapelekea madaraka kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Sifa muhimu zinazozitambulisha Serikali za Mitaa ni pamoja na:
Majukumu na kazi za jumla na za lazima za Serikali za Mitaa ziko katika Sheria za Serikali za Mitaa Sura 287 na 288 Toleo la 2002 awali Sheria Na 7 na 8 za mwaka 1982. Katiba ya Tanzania inaelekeza kwamba Serikali za Mitaa zitakuwa na madhumuni, majukumu na kazi kuu tatu zifuatazo:
(a) Kutekeleza majukumu ya Serikali za Mitaa katika maeneo ya mamlaka zao;
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na usalama wa wananchi; na
(c) Kuimarisha demokrasia katika maeneo yake na kuitumia katika kuongeza kasi ya maendeleo ya watu.
Kwa Kina zaidi soma hapa MAJUKUMU NA KAZI ZA MEYA-MWENYEKITI WA HALMASHAURI-MADIWANI-WENYEVITI WA VIJIJI-MITAA NA VITONGOJI.pdf
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.