Wilaya ya Ludewa pamoja na kuwepo kwa Ziwa Nyasa katika moja ya Tarafa zake zinazounda Wilaya hiyo, Tarafa ya Mwambao, ina mazingira rafiki kwa ufugaji wa samaki katika mabwawa. Shughuli hii inaweza kufanyika katika Tarafa zilizopo mbali kidogo na ukanda wa Ziwani, mathalani Tarafa ya Mawengi, Tarafa ya Liganga, Tarafa ya Mlangali na kwa kiasi Tarafa ya Masasi, kupitia Vikundi vya wajasiliamali, watu binafsi, taasisi au hata Serikali za vijiji. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wapo wadau wa ufugaji samaki ambao umevutia watu wengi pia kuingia kwenye shughuli ya kiuchumi ya namna hii. Mmoja wa wadau wa ufugaji wa Samaki ni Bwana Longinus Longinus Mgani anayepatikana katika Tarafa ya Liganga, Kata ya Lugarawa, Kijiji cha Mdilidili, Kitongoji cha Lusapo. Bwana Longinus Longinus Mgani ni Mzaliwa wa Wilaya ya Ludewa; yeye ni msomi katika ngazi ya Shahada ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ya mwaka 2015 hadi 2018. Amepata Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Matika, kati ya Mwaka, 2002 hadi 2008. Aliendelea na masomo ya Sekondari kidato cha kwanza hadi cha sita katika Seminari ya Mtakatifu Joseph Kilocha kati ya mwaka 2009-2012 na 2013-2015. Kutokana na Maarifa na Taaluma yake hiyo, amechaguliwa na Wananchi kuwaongoza akiwa kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumia maji, JUMALU (Water User Association Lugarawa Drainage Area ). Kwa sasa anajishughulisha na mradi wa ufugaji samaki katika mabwawa (Fish farm project) katika Kata ya Lugarawa, Kijiji cha Mdilidili, Kitongoji cha Lusapo akiwa na mabwawa takribani kumi na tatu. Kwa sasa yupo katika hatua za awali za samaki wadogo wadogo. Ni matumaini kwamba ataendeleza maarifa haya na kwa vijana wengine kupata ujuzi huu wa ufugaji samaki.
HABARI PICHA:
Picha mbalimbali za mabwawa ya Samaki anaofuga Bwana Longinus Mgani.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.