Katika kukabiliana na virusi vya Corona, vinavyosababisha homa ya mafua makali ya COVID-19, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imeungana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuzuia mikusanyiko ya aina yoyote kama ilivyoagizwa na Serikali. Badala yake, Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imetumia siku hiyo kuwaelemisha wananchi namna ya kukijinga na Virusi vya Corona, na kuhakikisha wanasimamia maagizo yote ya Serikali ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa Ujumla. Aidha Idara ya Maendeleo ya Jamii iliwasilisha Hotuba iliyoandaliwa na Mkoa ambayo ilikuwa imesheheni Elimu ya namna ya kupambana na virusi vya Corona. Kwa undani zaidi wa waliyosemwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa katika Hotuba hiyo, fungua hapa.HOTUBA YA MKUU WA MKOA SIKU YA FAMILIA.pdf
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.