Mradi unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa Ufadhiri wa Serikali Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Umetengewa Fedha Taslimu Kiasi cha Shilingi za Kitanzania Milioni Mia Tano. (Tsh. 500,000,000/=) mpaka kukamilika kwake.
Unatekelezwa kwa kutumia wataalamu wa ndani ambapo kunajengwa miundombinu ifuatayo;
1 Ujenzi wa Nyumba ya Kuishi Mtaalamu (Daktari).
2.Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto (Wodi ya Kina Mama)
3.Maabara kwa ajili ya vipimo mbalimbali vya Afya.
4.Chumba cha Upasuaji (Theater)
5.Chumba cha Kuhifadhi Maiti (Motuary)
Mradi umepangwa kukamilika katika muda wa majuma kumi na sita. Kukamilika kwake kunatarajiwa kuwa suluhu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wakazi wa Wilaya ya Ludewa, hususani wale wanaotokea katika tarafa za Mlangali na Liganga, kwani panatarajiwa kuwa na maboresho makubwa sana katika sekta ya afya katika Wilaya yetu.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.