Waziri Nape Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye (Mb) aliwataka maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati na kuacha utamaduni wa kusubiri mpaka taarifa za upotoshaji zitokee ndio watoe taarifa za kujitetea.
Waziri Nape aliyabainisha hayo jana Machi 29, 2023 wakati akizungumza katika kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
"Tuulishe umma taarifa sahihi na kwa wakati, ukiona inafikia hatua unatakiwa kutoa taarifa ya kujitetea basi ujue kuna mahali unakosea", Alisema Waziri Nape.
Aliongeza kuwa, "Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano ndio mmebeba taswira na mitazamo ya taasisi zenu, taswira na kutazama inatengenezwa hivyo ni wajibu wenu kutengeneza mitazamo chanya ya taasisi mnazotumika".
Alisisitiza kuwa, kada ya maafisa habari ina umuhimu wa kipekee na iwapo wakitimiza majukumu yaonipasavyo
wataongeza thamani na umuhimu wao katika taasisi wanazofanya kazi.
"Nimepokea changamoto zernu za bajeti na vitendea kazi, sasa nitoe wito kwenu wa kuhakikisha mnatimiza wajibu wenu ili ninapoenda kupigania haki zenu na nyie muwe mmeonesha
thamani ya uwepo wenu",
"Uafisa habari ni ajira, ni jukumu la kulinda taswira ya taasisi
yako, na pia ni fursa ya kubadili maisha binafsi na Taifa kwa
ujumla iwapo ukifanya vizuri katika eneo lako', alimasema Waziri Nape.
@chrispin_b__kalinga
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.