Afisa Mwandikishaji Ndg. Mathan Chalamila amewasisitiza Waandishi Wasaidizi ngazi ya Kata kuwa makini katika mafunzo watakayopewa ili waweze kusimamia zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa umakini. Aidha amesisitiza kutunza vifaa watakavyopewa katika mazingira mazuri na salama.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Sunday Deogratias aliyekuwa mgeni mwalikwa wa semina hii, amesisitiza kwamba elimu ambayo imetolewa itasaidia kutekeleza majukumu ya ujazaji fomu na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (voters registration system-VRS). Amesisitiza kusoma miongozo iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya uelewa zaidi.
Ikumbukwe kuwa zoezi la Uboreshaji wa daftari la Mpiga Kura litaanza tarehe 12 hadi 18 Januari 2025, na vituo vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni. Kila mwananchi anahimizwa kujiandikisha kwa muda uliopangwa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.