Mwenge wa Uhuru 2024 umeanza rasmi kukimbizwa ndani ya Wilaya ya Ludewa kwa kupitia miradi 7 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Mwenge huo umepokelewa tarehe 16 Juni 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva, kisha kuanza kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Mwenge wa Uhuru 2024 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa Ujenzi wa nyumba ya kulala wageni ya mjasiriamali ya Bw Alto Mkinga na Maradi wa maji Kata ya Mavanga Kijiji Cha Mavanga.
Pia umekagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa kituo cha afya Mundindi, Ujenzi wa chuo cha VETA Shaurimoyo na Mradi wa Upandaji Miti wa Ndugu Wilson Haule.
Mwenge wa Uhuru pia umefanya uzinduzi wa mradi wa Klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya sekondari ya UMAWANJO na Ujenzi wa barabara ya lami Lugarawa.
Aidha, Mwenge wa Uhuru ukiwa Ludewa umepokea taarifa ya mapambano dhidi ya malaria, UKIMWI, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Lishe na Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.