Na. Chrispin Kalinga - Ludewa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Afya na Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha ifikapo Januari 2024 kiwanda cha Dawa Idofi kilichopo Makambako mkoani Njombe upande wa dawa kiwe kimeanza kuzalisha licha ya kuzalisha gloves ili kuendelea kuleta tija kwa wananchi.
Mhe. Dkt. Mpango ametoa agizo hilo Jana tarehe 26 Oktoba, 2023 Mkoani Njombe mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza mipira ya Mikono (Gloves) kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa (MSD).
Alieleza kuwa, lengo la kiwanda hicho ni kuhakikisha wanaboresha Huduma kwa jamii na kuimarisha afya za wananchi kwa kuzalisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi hapa nchini.
Dkt. Mpango alisema kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi imara wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwezesha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa kuipatia mtaji Bohari ya Dawa ili kujenga viwanda zaidi vya dawa, maghala na kuongeza upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi nchini.
“Serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa lakini kwa kuwa uamuzi huo ni wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha hivyo vitajengwa kwa manufaa ya taifa"
“Kwa sasa serikali inaagiza dawa kwa asilmia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi, hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya, ni lazima kuchukua maamuzi magumu ili kuweza kujitengemea katika upatikanaji wa dawa nchini”. Alisema Dkt. Mpango.
Aidha alisema kuwa, Rais Samia ameamua viwanda vya dawa vijengwa kwa gharama yeyote kwa kuwa nchi ina uhaba wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.
“Tumeamua kuipatia MSD majukumu manne ambayo ni uzalishaji, ununuzi, utunzaji na usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi nchini hivyo ni niwahakikishie viwanda hivi vitajengwa nchini kwa maslahi ya taifa letu”, alisema Dkt. Mpango.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.