Katika Wilaya ya Ludewa, yapo maeneo watu hujishughulisha na Uchimbaji madini. Katika eneo hili, kuna maeneo ya kimkakati kama vile madini ya Chuma Liganga na Makaa ya mawe Mchuchuma. Lakini pia yapo maeneo mengine mengi ambayo wananchi kutoka pande zote za Jamhuri ya Muungano kwa njia rasmi na halali hufika kwa uchimbaji mdogo mdogo kama vile eneo maarufu la uchimbaji madini ya dhahabu katika Kijiji cha Amani kata ya Mundindi Wilayani Ludewa. Pia baadhi ya maeneo katika Kata ya Ibumi. Kwa taarifa zadi fika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya upate kujulishwa maeneo tajiri kwa madini ya vito katika Wilaya hiyo.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.