Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 Lt. Josephine Paul Mwambashi amekubali kuzindua miradi iliyopendekezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. Akizungumza na Wakazi wa Ludewa katika maeneo mbalimbali ambako Mwenge wa Uhuru umepita amesema kwamba ameridhishwa na namna utekelezaji wa Miradi hiyo ulivyofanyika na Hivyo anakubali kuizindua. Mradi wa kwanza ulikuwa wa Kituo cha Afya katika kata ya Lugarawa Kijiji cha Shaurimoyo unaotekelezwa kwa kiasi kikubwa kwa nguvu za wananchi ambao uliwekewa Jiwe la Msingi. Aidha aliweza kutoa hundi kwa kikundi cha watu wenye mahitaji maalumu kwa fedha za asilimia 10 ya wanawake, vijana na wenye ulemavu katika kijiji cha Mundindi kilichopo katika kata ya Mundindi. Pia Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 zilipita katika Shule ya Sekondari Lugarawa ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Lt. Josephine Mwambashi alizindua mradi wa ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa baada ya kuwa umekamilika. Kadhalika alizindua Nyumba ya kulala wageni ya Mwananchi wa Kata ya Lubonde katika kijiji cha Mkiu Ndg. Edger Mtitu. Katika Hatua nyingine, Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 katika eneo la Mkesha Kata ya Mlangali, Kiongozi wa Mbio za Mwenge alizindua Miundombinu ya Majengo ya Kituo cha Afya Mlangali yenye thamani ya takribani Tsh. 500,000,000/=. Pia alikagua Mfumo wa kuratibu matibabu na malipo Kielektroniki wa GoTHOMIS unaotumika katika Kituo cha Afya Mlangali. Sambamaba na Ukaguzi wa Mradi huu wa TEHAMA, alikagua pia shughuli za Lishe na Utoaji wa Chandarua katika mapambano dhidi ya Malaria.
Habari Picha:
Picha 1. Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Axwesso Tsere (anayesoma kabrasha) akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama katika Mapokezi ya Mwenge
Picha 2: Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Joseph Kamonga akijadiliana jambo na mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa kabla ya hafla ya makabidhiano na Wilaya ya Njombe
Picha 3: Habari picha ni katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Tsere na Mh. Kissa Gwakisa Mkuu wa Wilaya ya Njombe
Picha 4: Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Tsere (Kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mh. Kissa Gwakisa (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Njombe katika makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Kitulila kilichopo mpakani kati ya Wilaya hizo mbili.
Picha 5: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias (mwanzoni kabisa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ludewa katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.