Friday 19th, April 2024
@UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA
AWALI YA YOTE NAWASALIMU KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA;
KAZI IENDELEEEEEEE............
Ndugu Washiriki,
Nitumie fursa hii kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwepo hapa siku hii ya leo, pili niwashukuru washiriki wote kwa kuona umuhimu wa kikao hiki na mahudhurio mazuri hasa ukizingatia majukumu mengi tuliyonayo.
Napenda pia kuwashukuru Mkurugenzi Mtenfdaji wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Wilaya kwa kuratibu maandalizi ya kikao hiki muhimu.
Ndugu Washiriki,
Lengo kuu la kufanya kikao hiki ni kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Msingi (PHC) juu ya uanzishwaji wa chanjo dhidi ya janga la UVIKO 19 chanjo hii ni salama imethibitishwa na Mamlaka ya dawa na vifaa tibaTanzania na Mkemia Mkuu wa Serikali. Naomba tuunge mkono jitihada za Serikali na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuilinda jamii na magonjwa ya kuambukizwa ikiwemo UVIKO 19.
Ndugu Washiriki,
Makundi yatakayoanza kupata chanjo hizi ni Watumishi wa Afya, Wazee zaidi ya miaka 49, na wenye magonjwa sugu miaka 18 – 49 na huduma zitatolewa katika Hospitali ya Wilaya Ludewa, Hospitali ya Lugarawa, Hospitali ya Milo, Kituo cha Afya Manda, Kituo cha Afya Mlangali na Kituo cha Afya Makonde.
Ndugu Washiriki,
Kupitia kikao hiki muhimu mtajifunza kuhusu chanjo ya UVIKO – 19 ambayo tumepokea kwa ajili ya kuwakinga wananchi na janga la ugonjwa wa CORONA ili mtusaidie kuelimisha jamii na kuondoa mitazamo hasi iliyopo katika jamii inayotokana na mitandao ya kijamii juu ya Chanjo hii.
ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA.
HABARI PICHA:
Picha 1: Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere akizungumza katika kikao na wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi wakati akizindua zoezi la Chanjo dhidi ya UVIKO-19. Kulia kwake ni Ndg. Sunday N. Deogratius Mkurugenzi Mtendaji Wilaya akifuatiwa na Dr. Stanley Mlay Mganga Mkuu wa Wilaya.
Picha 2: Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Dr. Stanley Mlay akitolea ufafanuzi na Kuelimisha washiriki wa kikao masuala yanayohusiana na UVIKO-19 na Chanjo ya UVIKO-19
Picha 3: Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Andrea Tsere akipata chanjo ya UVIKO-19 katika zoezi la Uzinduzi wa chanjo hiyo Wilayani Ludewa.
Picha 4: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratius akiwa pamoja na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Bakari Mfaume (katikati) na OCD Ludewa Afande Massawe wakiwa katika foleni ili kupata Chanjo ya UVIKO-19 katika zoezi la uzinduzi wa chanjo Wilayani Ludewa
Picha 5: Viongozi wa Dini, Wataalamu wa Afya mbalimbali na wananchi wakiwa katika Kikao cha kupata elimu juu ya chanjo ya UVIKO-19
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.